Mwisho
I was looking at Nicholas Shiraku's drawing.............. and got inspired to write Mwisho. A story of a girl, who loved a man so much, she even got pregnant thinking that it would be a reason for him to stay with her but... he didn't! Mapenzi nimeshiba Nimeona hayana tiba Nimejitia kwa shida Nikikubebea mimba Sasa nalia msiba Uchungu unanilemea na moyo umenivunja Ukaniumiza uliposema nimekuwekea mtego Ukavibeba vyote vyako na kujionyesha mlango Ukajiona mwiko, kunilisha maringo Nimebaki na kilio nikilia mwisho! Kweli pendo lina mwisho… Mwisho! © Namatsi Lukoye