The Poet's Muse
Nayo iwe vipi
Kunimaliza kwa macho tu
Na ukinibusu… najishangaa tu
Nimekua kama zuzu napepea tu
Au labda kama mtoto nashindwa cha kufanya lo!
Nguvu gani jamani
Si kawaida nashuku ni vela au voodoo
Labda ni uchawi ulibeba toka pwani
Nawaogopa wanaokuja kama wewe - naogopa si mchezo!
Iwe vipi nawa mchenge
Mie pwagu iwe vipi nalemewa hivi
Macho yakikutana - yangu ya legea
Natamani ardhi ifunguke nijifichie
Najikaza najiwekea nanyamazia -
Mwili nao msaliti - jamani, vile moyo wapiga
Mwili wanisaliti - hata jinsi napumua
Mwili wanisaliti - maji hayo nishakua
and when you touch me
Za! Twende sasa!
Nipe yote kesho labda si yetu
Cheza nami usiogope kitu
Au labda tupande kwa majani tufike angani zetu
Una nguvu ajab, nikipi chanisumbua
Na wanimaliza huachi hata mfupa - umeninasa hongera mvuvi
Na wanimaliza huachi hata mfupa - umeninasa hongera mvuvi
Vidole kawa miguu, sasa basi tembea jua nchi
Zama kisimani - palipo madini labda almasi
Nawe kwa ujuzi - ule - mizizi hata mchuzi
Shanga kiunoni - nacho hakidanganyi
Kilivyo jilegeza - upate pa kushikilia
kilivyo jiachilia - upate pakusukumia
Wanasema ndio mwendo - mbona twende kasi
But tell me,
How long can you hold your breath!
Za!
Wanasema ndio mwendo - mbona twende kasi
But tell me,
How long can you hold your breath!
Za!
© Namatsi Lukoye
Comments
Post a Comment