The Poet's Muse
Nayo iwe vipi Kunimaliza kwa macho tu Na ukinibusu… najishangaa tu Nimekua kama zuzu napepea tu Au labda kama mtoto nashindwa cha kufanya lo! Nguvu gani jamani Si kawaida nashuku ni vela au voodoo Labda ni uchawi ulibeba toka pwani Nawaogopa wanaokuja kama wewe - naogopa si mchezo! Iwe vipi nawa mchenge Mie pwagu iwe vipi nalemewa hivi Macho yakikutana - yangu ya legea Natamani ardhi ifunguke nijifichie Najikaza najiwekea nanyamazia - Mwili nao msaliti - jamani, vile moyo wapiga Mwili wanisaliti - hata jinsi napumua Mwili wanisaliti - maji hayo nishakua and when you touch me Za! Twende sasa! Nipe yote kesho labda si yetu Cheza nami usiogope kitu Au labda tupande kwa majani tufike angani zetu Una nguvu ajab, nikipi chanisumbua Na wanimaliza huachi hata mfupa - umeninasa hongera mvuvi Vidole kawa miguu, sasa basi tembea jua nchi Zama kisimani - palipo madini labda almasi Nawe kwa ujuzi - ule - mizizi hata ...